Mandela: Mwanaharakati wa Ukimwi

Image caption Mandela alishtua Afrika Kusini alipotangaza kuwa mwanawe alifariki kutokana na Ukimwi

Ingawa mwanzoni hakuzungumzia sana maswala ya HIV, Nelson Mandela aliibuka na kuwa mwanaharakati mkubwa wa virusi vya HIV na maradhi ya Ukimwi.

Wakati aliachiliwa huru kutoka gerezani mwaka mwezi Februari, 1990,ugonjwa wa ukimwi, ulikuwa haujaanza kukita mizizi nchini Afrika Kusini.

Kufuatia kuchaguliwa kwake, miaka minne baadaye, Mandela alikabiliwa na changamoto kubwa sawa na viongozi wengine duniani wakati huo, ambao hawakuelewa vyema kuhusu maradhi ya ukimwi, na kwa hivyo hawakuwa na uelewa wala msaada wa kutosha kwa waathiriwa wakati huo.

Chama cha ANC, kilikuwa kimenaswa katika mjadala uliokuwa unaendelea kuhusu chanzo cha maambukizi ya HIV na matibabu ya ugonjwa wa Ukimwi.

Baadhi ya viongozi kama Thabo Mbeki, aliyemrithi Nelson Mandela, alihoji hadharini ikiwa kweli, virusi vya HIV husababisha maradhi ya ukimwi.

Baada ya Mandela kuondoka mamlakani, mnamo mwaka 1999, aliendeleza harakati za utafiti zaidi wa Ukimwi kufanywa, akatoa wito wa elimu , ngono salama, na matibabu kwa wale walioathiriwa.

Hata hivyo, Raia wengi wa Afrika Kusini bado hawakutaja maradhi hayo hadharani.

Kwa mujibu wa UN, takwimu zinaonyesha kuwa idado ya watu wazima walioambukizwa virusi vya HIV, ilipanda kutoka asilimia 1 mwaka 1990 hadi 17.9 mwaka 2012.

Afrika Kusini ni moja ya nchi zenye viwango vya juu Zaidi vyaa maambukizi ya HIV duniani.

Kadhalika Afrika Kusini ina Idadi kubwa ya watu wanaoishiri ni virusi vay HIV duniani. Watu milioni 6.1 walijulikana kuishi na visrusi vya HIV mwaka 2012, ikiwemo watoto 410,000 walio chini ya umri wa mwaka mmoja hadi miaka 14. Nchi hiyo ina watu milioni 51.

Wataalamu wamekuwa wakisema kuwa sababu moja kuu ya viwango hivi vya maambukizi ni umaskini na tamaduni ambazo zinahatarisha maisha na umaskini miongoni mwa wanawake.

Mbali na masaibu yanayotokana na virusi vya HIV, athari za kiuchumi ni mbaya zaidi hasa uchumi wa Afrika Kusini unapoendelea kudumaa.

Mandela hata hivyo alianza kuzungumzia Zaidi Ukimwi alipoondoka mamlakani mwaka 1999.

Wakati dunia ilipoadhimisha siku ya ukimwi duniani, mwaka 2000, Mandela alituma ujumbe mkali sana akisema Afrika Kusini inakabiliana na janga la Ukimwi.

'' Tunakabiliwa na adui mbaya sana ambaye anatishia kuangamiza jamii yetu.''

''Tafadhani muwe na mpenzi mmoja na mtumie Condom........tafahdali tuwapende watoto na kuwapa maisha mema na amani sio Ukimwi,'' alisema Mandela

Alisema nchi yake, lazima iendeleze kampeini ya watu kujizuia na ngono , watumie condom na wapokee matibabu pamoja na kupata ushauri nasaha sawa na kuzuia maambukizi kutoka kwa mama hadi kwa mtoto.

Wakati huo wote, serikali ya Afrika Kusini haikujitolea sana katika kufadhili matibabu kwa waathiriwa.

Image caption Kifo cha Mandela kimewagusa watu wengi duniani

Mwanawe Mandela alifariki kutokana na Ukimwi mwaka 2005.

Naye aliyekua rais Thabo Mbeki akawaghadhabisha wengi kwa kusema kua yeye hamjui mtu yeyote aliyefariki kutokana na ugonjwa huo na wala hakumbuki kama amekutana na mtu yeyote aliyeambukizwa HIV.

Mmoja wa mawaziri wake naye akapendekeza kua watu wale Kitunguu Saumu ili wapunguze makali ya Ukimwi.

Mnamo mwaka 2003, Mandela alizindua wakfu wake wa kupambana na ukimwi na kuchangisha pesa kwa ...kampeini hiyo ilijulikana kama 46664, nambari yake apokua gerezani.

Wakati mmoja Mandela alilinganisha vita dhidi ya ukimwi sawa na vita dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo.

Kampeini hiyo ilipata ufadhili zaidi mwaka 2005 wakati Mandela aliposhtua taifa hilo kwa kusema mwanawe Makgatho,alifariki kutokana na ukimwi.

Mandela aliwataka watu wazungumzie ukimwi ili kuufanya kuonekana kama ugonjwa wa kawaida.