Mwandishi wa BBC amkumbuka Mandela

Image caption Mandela aliwagusa watu wengi duniani

Nelson Mandela alijiondoa kutoka maisha ya umma mwaka 2004. Mwandishi wa BBC Richard Hamilton alikuwa mwandishi wa BBC mjini Cape Town wakati huo na anatuletea kumbukumbu zake kuhusu rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini:

"Bwana Mandela, unawezaje kuwa katika hali hii nzuri ya mwili? Aliuliza ripota msichana wa tv, ambaye aligongana jicho na Bwana Mandela.

Tulikuwa katika eneo la gereza la Kisiwa cha Robben ambako Nelson Mandela alitumikia miaka kumi na nane kati ya ishirini na saba aliyofungwa jela.

Mkutano wa waandishi wa habari wa kuzindua tamasha la 46664 la kupambana na Ukimwi.

Wasanii nyota wa muziki wa rock na watu maarufu wakiwemo Bono, Beyonce na Annie Lennox - walijipenyeza katika ukumbi huo kumsikiliza mtu mashuhuri akizungumza.

Nilisikia kusisimka mgongo na kupaliwa kooni nilipomwona kwa mara ya kwanza, akitembea taratibu kutoka katika mlango akishuka ngazi. "Vema," alijibu akisita makusudi akiwa na bashasha usoni "hilo ni suala binafsi."

Hadhira ilianguka kicheko. Kama jambo la ziada, Mandela alisema, niliona kuwa pombe ya Cuba inasaidia sana."

Ilikuwa ni hali hii ya ucheshi ambayo ilimfanya Nelson Mandela kuwa kipenzi cha watu wengi.

Miezi sita baada waandishi wa habari walikusanyika katika Kisiwa cha Robben. Mwenge wa Olympiki ulikuwa njiani kuelekea Athens, Ugiriki na Mandela alipewa jukumu la kuushika.

Umati ulianza kufurika wakati wapiga picha walipokuwa wakitafuta sehemu nzuri zaidi ya kuchukua picha, mzee aliyumba kidogo na kwa sekunde fulani alionekana kana kwamba mwenge huo wa Olympiki ungeanguka.

"angalia mwenge" alipiga kelele mwandishi mmoja. "usijali kuhusu mwenge, " alisema Mandela kwa kutania, "inabidi ujali zaidi kuhusu mimi." Lakini hatukushitushwa nae.

Tulijua kuwa alikuwa mzee lakini tulifikiria alikuwa mtu asiyeyumbishwa na angendelea kwa miaka kadhaa. Sikutambua hilo wakati huo lakini wakati huo ulikuwa wa mwisho kwake kujitokeza katika shughuli maalum za kijamii.

Si muda mrefu sana kutoka wakti huo, alijiondoa katika maisha ya umma, akiwa bado na ucheshi ule ule akitoa maneno: "usinite, nitakuita."