Dakika za mwisho za maisha ya Mandela

Image caption Mwanawe Mandela Makaziwe Mandela

Huku bunge la afrika kusini likifanya kikao maalum cha kumheshimu mandela ,mwanawe mkubwa wa kike Makaziwe ameiambia BBC kuhusu dakika za mwisho za maisha ya babake.

Amesema kuwa ijapokuwa hakuwa akifungua macho mara kwa mara,alikuwa na uhakika kuwa aliweza kusikia vile familia yake ilivyompenda.

Makaziwe amekiri kuwa hakuweza kuwasiliana vyema sana na babake na kwamba babake hakuweza kuonyesha hisia zake,lakini yote hayo alitaka familia yake kupatana.

Amesema kitu kikubwa alichoelimishwa na babaake ni kuwa na ujasiri wa kusamehe.