Unicef:'Ni kosa watoto hawaandikishwi'

Image caption Unicef

Shirika la kushughulikia maslahi ya watoto duniani la Unicef, limesema kuwa takriban watoto milioni laki mbili na thelathini hawajawahi kuandikishwa tangu wazaliwe.

Hiyo ina maana kuwa katika kila watoto watatu wenye umri chini ya miaka mitano duniani kumbukumbu zake hazipo popote.

Aidha Unicef inasema kuwa vyeti vya usajili, vinamhakikishia mtoto kuwa hatawahi kusahaulika, kunyimwa haki zake au kunyimwa huduma muhimu kama afya au elimu.

Utafiti huo uliofanywa katika nchi miamoja na sitini na moja, uligundua kuwa Afrika Kusini ndio nchi mojawapo yenye idadi kubwa ya watoto kutoandikishwa pindi wanapozaliwa Kusini mwa jangwa la Sahara.

Shirika hilo hata hivyo limesema Uganda imepiga hatua katika kuwaandikisha watoto ambapo inatumia simu za mkononi kuwaandikisha watoto na kutumia muda mfupi sana badala ya miezi mingi kama ilivyokuwa hapo nyuma.