Kenya yakata keki miaka hamsini!

Kenya inafikisha miaka hamsini Alhamisi hii tangu kujitatawala miaka hamsini iliyopita.

Kumbukumbu , maoni, mageuzi, yote haya na mengi mangineo yanajitokeza katika umuhimu wa kusherehekea mwaka huu wa Jubilee.

Kumbukumbu

Mnamo mwaka 1998, watu 224 walifariki wakati kundi la kigaidi la Alqaeeda liliposhambulia ubalozi wa Marekani nchini Kenya .

Wakati huu ambapo Kenya inafikisha umri wa makamo, ni jambo la kawaida kwa watu kusahau baadhi ya vitu. Unaweza kupoteza funguo zako, hata usahau filamu uliyoitizama mwezi jana, Kenya pia inaonekana kusahau haraka.

Kabla ya mashambulizi ya kigaidi kufanyika dhidi ya jengo la Westgate mjini Nairobi mwezi Septemba ambako mamia walijeruhiwa na wengine kuuawa, Kenya iliwahi kukabiliana na hali kama hii, mashambulizi mabaya zaidi hata kuliko ya Westgate ambayo yalilenga ubalozi wa Marekani mjini Nairobi.

Lakini mafunzo ambayo Kenya ingetoa kwa mashambulizi ya kigaidi yakawa yamesahahulika.

Maono

80% ya wakenya wako chini ya umri wa miaka 35.

Mabadiliko katika umri yanapaswa kuleta mabadiliko katika maono.

Tunapoendelea kuzeeka, Kenya inahitaji miwani kuona vyema zaidi.

Kisheria Kenya inaonekana kuzeeka kabisa.

Na nchi inapoendelea kuzeeka imekosa kuona kuwa idadi ya vijana inaongezeka maradufu

Asilimia themanini na wakenya wako chini ya umri wa miaka 35, na kila mtoto anapozaliwa, anahitaji kupangiwa elimu, kulishwa, huduma ya afya na ajira. Lakini licha ya idadi ya watu kuongezeka, ni vijana ambao wanakabiliwa na changamoto ya ajira.

Idadi ya watu Kenya imeongezeka zaidi ya mara nne tangu nchi hiyo kujipatia uhuru.

Asilimia 42% wako chini ya umri wa miaka 15. Idadi ya watoto wanaofariki wakizaliwa imepungua. Vijana hawana ajira na hao ndio wengi zaidi. Kenya inahitaji kuona vyema inachohitaji kufanya kubadili hali wakati inaposherehekea miaka hii hamsini ya Uhuru wake.

Harakati

Kumekuwa na maandamano ya kila aina kuonyesha ghadhabu juu ya wabunge kujiongeza mishahara mwaka huu.

Serikali haikusikia kilio hicho na wabunge waliweza kupata walichokuwa wanataka.

Kabla ya uchaguzi mwezi Machi, wananchi waliandamana kwa hasira wakiwalaani wabunge waliokuwa wanawaibia pesa zao ili kujipa maisha mema, lakini kwa hofu ya kutopigiwa kura , waliamua kutojiongeza mishahara hiyo wakati huo hadi pale uchaguzi ulipokamilika.

Serikali haikusikia kilio cha wananchi , wabunge sasa wako sawa maana walikipata walichokitaka.

Yote tisa, kumi ni kuwa Kenya inaposherehekea miaka hamsini ya uhuru wake, kuna mengi ambayo serikali inaendelea kupuuza . Na kwa mwananchi wa kawaida itachukua muda labda miaka mingine hamsini kwake kuona mafanikio ya juhudi za wakombozi na wazalendo waliopigania uhuru.