CAR tayari kwa mazungumzo na waasi

Image caption Michel Djotodia aliingia mamlakani baada ya kupiundua serikali ya Francois Bozize

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Michel Djotodia amekubali kufanya mazungumzo na viongozi wa makundi ya wapiganaji wa kikrsto wanaohangaisha wananchi kwa misingi ya kidini.

Kwa sasa hali inaendelea kuzorota kutokana na vita vya kidini.

Kupitia kwa kituo cha redio cha kifaransa RFI , Rais Djotodia amesema yuko tayari kushauriana na wapiganaji hao.

Rais Djotodia ambaye ni kiongozi wa zamani wa waasi, aliingia mamlakani baada ya kufanya mapinduzi mwezi Machi na kumuondoa mamlakani aliyekuwa rais muisilamu Francois Bozize mnamo mwezi Machi.

Mamia ya watu wameuawa kwenye ghasia za kidini kuanzia mwezi Disemba.

Wapiganaji hao wanasema Rais tayari Djotodia amesema kuwa kuwa wao sio maadui bali ndugu zake na kuwa wanaweza kujumuishwa katika serikali.

Matamshi yake yanakuja siku moja baada ya Muungano wa Afrika kuidhinisha wanajeshi zaidi kwenda Mali kukabiliana na wapiganaji hao.

Wanajeshi hao wa AU pamoja na wengine 1,600 kutoka Ufaransa, wanajaribu kurejesha utulivu nchini Mali pamoja na kuwapokonya silaha wapiganaji hao ambao wanadhibiti sehemu kubwa ya nchi.

Jamhuri ya Afrika ya kati, ilitumbukia katika vita vya kidini baada ya Rais Djotodia kupindua serikali ya aliyekuwa Rais Francois Bozize.

Lililokuwa kundi la waasi la Seleka ambalo lilikuwa linaunga mkono Djotodia sasa limeacha uasi lakini wapiganaji wake wangali hawajulikani waliko huku wakituhumiwa kwa kufanya maasi dhidi ya jamii ya wakristo.

Wapiganaji wa kikristo nao inasemekana walichukua silaha katika hatua ya kulipiza kisasi.