Polisi wafukuzwa kwa rushwa Uturuki

Image caption Recep Tayyip Erdogan Waziri mkuu wa Uturuki

Polisi waandamizi watano nchini Uturuki wamefukuzwa kazi kutokana na tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa.Hatua hii ya kufukuzwa kwa polisi hao ni matokeo ya kushikiliwa kwa watu Zaidi ya 20 kwaajili ya uchunguzi Zaidi kutokana na kutuhumiwa kuhusika na rushwa

Walioshikiliwa kwa tuhuma hizo ni pamoja na watoto wa mawaziri wa serikali,maafisa wa serikali na wafanyabiashara wanaodaiwa kuwa karibu na waziri mkuu wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan.

Taarifa toka nchini humo zinaarifu kuwa kuna dalili za mgawanyiko mkubwa ndani ya serikali hiyo chini ya chama tawala cha AK kati ya Waziri mkuu Erdogan na makundi ya kiislam yanayoongozwa na Fethullah Gulen.

Polisi hao waliofukuzwa baadhi yao wanadaiwa kuhusika katika kashfa hiyo