Watu 40 wauawa Mashariki mwa DRC

Image caption Wanajeshi wa DRC mjini Goma

Ripoti kutoka Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo zinasema kuwa idadi kubwa ya raia wameuawa kufuatia shambulio lililotokea mjini Kamango.

Habari ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa idadi ya waliouawa ni watu arubaini.

Msemaji wa shirika la Kimataifa la Msalama Mwekundu ICRC, amesema waliojeruhiwa wamepelekwa Goma kwa matibabu.

Amesema shirika la msalaba mwekundi nchini Congo linaendelea na shughuli ya kusaidia katika harakati za kuwazika waliouawa kwenye mapigano hayo.

Jeshi la Congo lina kambi mjini Kamango ambalo limekuwa likishambuliwa na wanamgambo wa waasi mara kwa mara, wakiwemo waasi wa Kiislamu kutoka Uganda wanaohudumu nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.