Polisi wagundua bomu jingine

Vyombo vya usalama nchini Misri vimeelezea kubaini mbinu zilizotumika kutega bomu lililolipua basi la abiria katika Jimbo la kaskazini katika mji wa Nasr nchini humo

Polisi wanasema kuwa bomu hilo lilitegwa kando ya barabara eneo la watembea kwa miguu na lililipuka mara tu basi hilo la abiria lilipokaribia eneo hilo

Idara za usalama zimeiambia BBC kuwa wataalamu wa milipuko wamegundua kuwa kulikuwa na bomu jingine lililokuwa limetengwa karibu na kwenye ubao wa matangazo hatua chache kutokea pale lilipolipuka la kwanza

Shambulizi hili la bomu limetokea huku siku ya jumanne wiki hii kukiwa na mlipuko mwingine wa bomu ndani ya gari katika jingo la walinzi kaskazini mwa mji wa Mansoura ambapo watu 16 walifariki dunia na wengine 100 kujeruhiwa

Serikali inalituhumu kundi la Muslim Brotherhood kuhusiaka na tukio hilo japo kuwa kundi hilo limekanusha madai hayo. Kundi la wapiganaji wa kiislam linalodaiwa kushirikiana na kundi la kigaidi la al qaeda la Ansar Beit al-Maqdis (Champions of Jerusalem) limekiri kuhusika na shambulio hilo