Vijana wa Riek Machar wanaelekea Bor

Raia wakikimbia mnapigano ya Bor

Maelfu ya vijana wa Sudan Kusini wanaompendelea Riek Machar, wanasemekana kuwa wanaandamana hadi mji muhimu wa Bor, mji mkuu wa jimbo la Jonglei.

Wanajeshi wa serikali wanadhibiti mji wa Bor baada ya kuukomboa kutoka kwa wanajeshi walioasi, huku mapigano ya kikabila yanaendelea nchini.

Vijana hao wa kabila la Nuer wanajulikana kama White Army (Jeshi Jeupe), kwa sababu ya jivu jeupe wanalojipaka kujikinga na wadudu.

Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini ameielezea BBC kwamba wanajeshi wake wanapigana kujaribu kudhibiti visima vya mafuta katika jimbo la Unity, kaskazini mwa nchi.

Ijumaa, Bwana Machar alisema wanajeshi wake wanadhibiti jimbo zima la Unity na jimbo lote la Jonglei, nje ya mji mkuu wa jimbo, yaani Bor.