Kamanda wa DRC auawa vitani Kivu

Image caption Kamanda Ndala aliuawa baada ya kuviziwa na waasi wa ADF-Nalu

Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Lambert Mende, amesema kuwa kamanda wa majeshi ya serikali yanayopigana dhidi ya kundi la wapiganaji wa kiisilamu wa Uganda, mashariki mwa nchi ameuawa.

Kanali Mamadou Ndala alifariki baada ya kuviziwa na waasi katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Waasi wa ADF-Nalu ndio waliofanya shambulizi hilo.

Kanali Ndala alihusika katika juhudi za kijeshi dhidi ya kundi la waasi wa M23 mwezi Novemba mwaka jana na hasa aliongoza kikosi cha jeshi dhidi ya waasi hao wa ADF-Nalu.

Jeshi la Congo, likiungwa mkono na wanajeshi wa Umoja wa mataifa linapambana na makundi ya waasi waliojihami Mashariki mwa nchi.

Eneo hilo linapakana na Uganda, Rwanda na Burundi.