Tunisia kupata katiba mpya

Image caption Sokomoko limeshuhudiwa Tunisia zaidi tangu wanasiasa wawili kuuawa mwaka jana

Wabunge nchini Tunisia wameanza kupigia kura rasimu ya katiba mpya ambayo ilipaswa kupitishwa muda mrefu umepita.

Aidha wataipigia kura kipengee kimoja baada ya kingine na sharti katiba yenyewe iwe imeidhinishwa ifikapo tarehe 14 mwezi Januari....ambao utatimiza mwaka wa tatu kuadhimishwa kwa mapinduzi ya kiraia yaliyofanyika nchini humo mwaka 2011

Katiba mpya itakuwa hatua kubwa katika kipindi cha mpito cha demokrasia nchini humo.

Imechukua zaidi ya miaka miwili kwa wabunge kukubaliana kuhusu rasimu ya katiba.

Wengi wanatumai kuwa kupitishwa kwa katiba hiyo kutamaliza hali ya sintofahamu kati ya mirengo tofauti ya kisiasa.

Mauaji ya wanasiasa wawili wakubwa mwaka jana ilitumbukiza nchi hiyo katika mgogoro wa kisiasa