Sudan. K:Serikali na waasi wazungumza

Image caption Rais Bashir na Kiir wamekutana kuzungumzia swala la ulinzi wa mabomba ya mafuta

Mazungumzo kati ya serikali ya Sudan Kusini na kundi la wanajeshi waliojitenga yameanza ili kukomesha mapigano.

Waziri wa habari Michael Makuei amesema kuwa swala la wafungwa wa kisiasa yameibuliwa. Pande zote mbili zimezungumzia hitaji la kukomesha mapigano, lakini serikali imesema kuwa wanajeshi wake wanazidi kuisogelea mji wa Bor.

Wapatanishi wawili wameondoka kwenye mkutano wa mazungumzo unaofanyika Nchini Ethiopia ili kuzungumza moja kwa moja na Rais Salva Kiir katika mji mkuu wa Sudan Kusini Juba.

Awali Mpatanishi mkuu upande wa waasi kwenye mgogoro wa Sudan Kusini, alitoa wito wa kuwepo suluhu la kisiasa akisema kuwa ndilo jibu la kipekee kwa mzozo huo.

Mpatanishi huyo (Taban Deng Gai) alitoa matamshi yake katika mazungumzo ya amani yanayoendelea kati ya pande zinazozozana mjini Addis Ababa Ethiopia.

Mwakilishi wa serikali Michel Makuel, alisema kuwa upande wa serikali umejitolea kuhakikisha kuna amani na kuwamba vifo vinavyosababishwa na mapigano sharti vikome.

Makabiliano kati ya upandea serikali ya Rais Salva Kiir na waasi wanaoongozwa na aliyelkuwa makamu wa Rais Riek Macahr, yamesababisha maelfu kutoroka makwao.

Awali, viongozi wa Sudan na Sudan Kusini, ambao wakati mmoja walikuwa mahasimu wakuu wa kisiasa wakati wa vita vya uhuru wa Sudan Kusini, walikutana kujadili , kutumia kikosi cha pamoja kulinda visima na mabomba ya mafuta Sudan Kusini dhidi ya kutekwa au kuharibiwa na waasi wakati vita hivi vinapoendelea.