Mateka 50 wauawa Syria

Image caption Wadadisi wanasema vita vya Syria havionekani kukaribia kukoma

Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu katika mji wa Alepo kaskazini mwa Syria, wanasema kuwa wapiganaji wanaoshukiwa kuhusishwa na kundi la Al-Qaeda wanadaiwa kuwauwa karibu mateka 50 waliokuwa wamewazuilia

Waliouwawa wanasemekana kujumuisha Matabibu, wanahabari na wafuasi wa kundi hasimu la waasi.

Aidha mauwaji hayo hayajathibitishwa.

Kundi hilo la wapiganaji wa kiislamu kutoka Iraq linalojulikana kama ISIS limekuwa likipigana na muungano wa waislamu walio na msimamo wa kadri mjini Aleppo.

Muungano huo unaishutumu ISIS linalojumuisha waislamu wa kigeni wenye itikadi kali ya vita vya Jihad kwa kuuteka vugugu hilo dhidi ya Rais Bashar Al-Assad.