4 wafariki kwenye ajali ya Helikopta US

Image caption Eneo la Norfolk ilipoanguka Helkopita ya Jsehi la Marekani

Helikopta ya Jeshi la Marekani imeanguka na kuua watu wanne katika pwani ya Norfolk ambako wanajeshi wa jeshi anga la Marekani walikuwa katika mazoezi.

Taarifa zinaeleza kuwa helikopta hiyo yenye namba HH-60G aina ya Pave Hawk ilikuwa imebeba zana za kivita na ilitaka kutua eneo la mchanga ufukweni mwa bahari kaskazini mwa kambi ya jeshi ya Norfolk.

Suzanne McKnespiey ni mmoja wa wafanyabiashara karibu na eneo la Norfolk anasema walisikia mlio mkali wa ndege hiyo kisha wakaona helikopta ikizunguka ovyo baharini na baadaye kishindo kikubwa.

Vikosi vya uokoaji na wanajeshi bado wapo katika eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi zaidi huku raia wakiwa wamezuiwa kufika katika eneo hilo kwa usalama wao dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mabaki ya silaha zilizokuwa katika helikopta hiyo.

Eneo lenye ukubwa wa mita 400 katika pwani hiyo ya Norfolk limewekewa vizuizi, ambapo afisa wa polisi Sarah Hamlin wa kituo cha polisi cha Norfolk, ametahadhalisha raia kutofika eneo hilo kipindi hiki cha uchunguzi.