Huwezi kusikiliza tena

Maelfu wakimbia vita Sudan Kusini

Waasi nchini Sudan Kusini wameanza harakati za kuulinda vikali mji wa Bentiu ambao waliutwaa kutoka kwa serikali wakihofia majeshi ya Serikali kuupigania.

Takriban Watu 1,000 wameuawa katika mapigano nchini humo huku wengine takriban 200,000 wakikimbia mapigano kati ya Jamii ya Dinka na Nuer.

Serikali kadhaa ulimwenguni zimewaondoa Raia wake waliokuwa Sudani kusini, huku raia wa nchini humo pia wakivuka mipaka kwenda nchi za jirani kutafuta hifadhi.