Machar akutana na mjumbe wa Marekani

Riek Machar

Taarifa ya waasi wa Sudan Kusini inasema kuwa mjumbe wa Marekani, Donald Booth, pamoja na wapatanishi wa kanda ya Afrika Mashariki, wamezungumza na kiongozi wa waasi hao, Riek Machar.

Taarifa hiyo iliyopokewa na shirika la habari la Ufaransa ilieleza kuwa mazungumzo hayo yalifanywa Jumamosi lakini haikutaja yalifanywa wapi.

Taarifa imetiwa saini na Miyong G Kuon, afisa wa habari wa Bwana Machar.

Hakuna mtu mwengine aliyethibitisha habari hizo.

Mazungumzo ya amani nchini Ethiopia ambayo yanalenga kumaliza majuma mane ya vita nchini Sudan Kusini hayaoneshi kuwa yamepiga hatua.

Inaonekana kizuiizi kikubwa ni shuruti ya Bwana Machar kuwa wafuasi wake 11 waachiliwe huru mjini Juba.