S.Kusini: Mazungumzo yakwamuliwa klabuni

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mapigano nchini Sudan Kusini yamewaacha maelfu bila makao na kukimbilia nchi jirani

Wajumbe katika mazungumzo ya kupatanisha pande zinazozozana kwenye mgogoro wa Sudan Kusini, wameachwa vinywa wazi baada ya kupewa klabu ya disco kufanyia mazungumzo kutokana na ukosefu wa vyumba vya kutosha katika hoteli ya kifahari ya Sheraton, mjini Addisa Ababa , Ethiopia.

Klabu ya Gaslight ndiko kunakofanyika mazungumzo hayo.

Na hii ni baada ya chumba walichokuwa wanatumia wajumbe hao katika hoteli ya kifahari ya Sheraton kutumiwa na wanadiplomasia wa Japan.

Duru zinasema kuwa baadhi ya wajumbe waliudhika kutokana na ukosefu wa mwangaza wa kutosha pamoja na kelele nyingi.

Klabu ya The Gaslight iko kwenye chumba cha chini ya hoteli ya Sheraton, na ni klabu mashuhuri ambayo hutembelewa tu na watu mashuri,matajiri pamoja na wasichana vipusa.

Katika siku ya kawaida, wanadiplomasia na wafanyakazi wa mashirika yasiyo ya kiserikali hufurika kwenye klabu hiyo.

Mazungumzo yanayonuiwa kusitisha vita ambavyo vimekuwa vikiendelea kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa, yameanza tena , lakini wajumbe wanakutaka katika chumba cha chini ya hoteli ya Sheraton ambapo kuna kilabu ya disco.

Chumba walichokuwa wanatumia awali kabla ya mzungumzo kukwama, kinatumiwa na waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe ambaye yuko kileleni mwa ziara yake ya kwanza Afrika.

Mazungumzo hayo, hata hivyo yatakuwa yanafanyika nyakati za mchana wakati angalau kelele sio kingi sana.

Mazungumzo hayo yanaongozwa na shirika la Igad.

Wajumbe wanatumai kuwa wataweza kupata mwafaka wa kusitisha vita hivyo ambavyo vimesababisha vifo vya watu, 1,000.

Mogogoro huu kati ya Rais Kiir na aliyekuwa makamu wake wa Rais Riek Machar, ulianza Disemba kumi na tano