Kauli yako: Katiba ndio suluhu Misri?

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mabango mengi yemekuwa yakiwashawishi wananchi kupiga kura ya ndio

Wananchi wa Misri leo wanapigia kura katiba mpya.

Je unadhani ndio itakuwa suluhu la kisiasa kwa nchi hiyo inayoyumba kisiasa?

Misri imekuwa ikitetereka kisiasa tangu kufanyika mapinduzi ya Kiraia yaliyomwondoa mamlakani Hosni Mubarak na kisha Rais aliyechaguliwa kidemokrasia Mohammed Morsi akaondolewa mamlakani na jeshi.

Je suluhu la kisiasa misri liko kwenye katiba mpya?

Tupe maoni yako kupitia ukurasa wetu wa Facebookbbcswahili

14:06 :Iddi Pesambili ana sema Sio suluhisho mpaka viongozi watakao kua madarakani wakubali kufuata matakwa ya viongozi wa Magharibi

14:04 :Owembabazi Edward Junior akiwa Makerere Uganda, anasema kupitia ukurasa wetu wa facebook kuwa katiba mpya haitakuwa suluhisho kwa sababu nayo wataivunja.Misri itaendelea kuwa nchi ya mizozo kati ya serikali na kikundi cha 'Muslim Brotherhood' ambao wanawachukua kuwa magaidi.'Niko hapa Chuoni Makerere.