Msaada wa dharura unahitajika Syria

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Umoja wa Mataifa unahitaji dola bilioni 6.5 kuwasaidia watu wa Syria

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anasema kuwa nusu ya wananchi wa Syria wanahitaji msaada wa dharura wa kibindamau.

Syria ina watu milioni 9.3.

Bwana Ban alikuwa akiongea kwenye mkutano wa wahisani nchini Kuwait ambapo kampeini kubwa zaidi ya msaada kwa watu wa Syria ilizinduliwa.

Umoja wa Mataifa unahitaji dola bilioni 6.5 wakati imeweza tu kuchangisha dola bilioni 2.4 mwishoni mwa Jumatano.

Wakati huohuo, naibu waziri wa mambo ya nje wa Syria amesema kuwa maafisa wa ujasusi kutoka katika dola za kimagharibi wamefanya mkutano na serikali ya Syria kuhusu kupambana na makundi ya wapiganaji wa kiisilamu.

Ushawishi wa makundi hayo miongoni mwa waasi wanaopigana na serikali ya Rais Bashir, umezorotesha mgogoro huo zaidi na kusababisha wasiwasi katika jamii ya kimataifa.