Vatican kujieleza kuhusu kashfa za ngono

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Papa Francis amaesema kuna haja ya kukabiliana na tatizo la dhuluma za kingono kanisani

Maafisa katika Vatican makao makuu ya kanisa katoliki, wanatarajariwa kuhojiwa na maafisa wa Umoja wa Mataifa kuhusu dhuluma za kingono ambazo makasisi wa kanisa hilo waliwatendea maelfu ya watoto.

Maafisa hao walikataa ombi la awali ambapo Umoja wa Mataifa ulikuwa unataka taarifa za kina kuhusu dhuluma za kingono wakisema kuwa visa hivyo vinapaswa kushughulikiwa na idara ya mahakama katika mataifa ambako visa hivyo vilitokea.

Papa Francis amesema kuwa ni jambo muhimu kukabiliana na visa kama hivyo ili kanisa liweze kupata sifa yake nzuri.

Kanisa hilo limekosolewa kwa kukosa kuchukua hatua za kutosha kuhusiana na madai ya dhuluma za kingono kanisani.

Mwezi jana, Papa Francis alitangaza kubuni kamati ya kukabiliana na visa vya dhuluma za kingono dhidi ya watoto kanisani pamoja na kutoa ushauri nasaha kwa waathiriwa.

Pia alitilia mkazo sheria kadhaa za kukabiliana na watuhumiwa wa dhuluma za kingono na kupanua zaidi maana ya uhalifu.