Maafisa wa UN na IMF wauawa Kabul

Haki miliki ya picha AP
Image caption Maafisa wa usalama wakiwasili katika eneo la tukio la shambulizi mjini Kabul

Takriban watu 15 wameuawa mjini Kabul nchini Afghanistan baada ya mlipuaji wa kujitoa mhanga kushambulia mkahawa mmoja wa ki-lebanon unaopendwa na raia wa kigeni pamoja na maafisa wa serikali.

Afisaa mmoja mkuu wa shirika la Fedha duniani tawi la Afghanistan Wadel Abdallah pamoja na maafisa wengine wanne wa Umoja wa Mataifa ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha yao.

Maafisa wa polisi wanasema kuwa mshambuliaji huyo alijilipua katika mlango wa mkahawa huo katika sehemu ya mji huo ilio na watu wengi.

Watu wawili waliojihami kwa bunduki baadaye waliwafyatulia risasi waathiriwa wa mlipuko huo.

Kundi la wapiganaji wa Taleban limekiri kutekeleza shambulio hilo.