Kaimu Rais CAR aelezea matumaini

Haki miliki ya picha AP
Image caption Samba Panza alichaguliwa na wabunge

Rais mpya wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema kuwa ana matumaini anaweza kurejesha utulivu na amani nchini humo.

Kwenye mahojiano na BBC , Bi Catherine Samba-Panza amesema kuwa serikali inahitaji kuhamasisha watu kuhusu umuhimu wa kuishi pamoja kwa amani na lazima wasitishe ghasia za kidini.

Rais huyo wa mpito pia ametoa wito wa kupelekwa wanajeshi zaidi nchini humo.

Bi Samba-Panza, ambaye ni wakili na meya wa zamani wa mji mkuu Bangui, alichaguliwa na wabunge siku ya Jumatatu, kama kaimu Rais.

Maelfu ya watu wameuawa katika mapigano kati ya waisilamu na wakristo tangu mapinduzi ya kijeshi kufanywa Machi mwaka jana.