Uganda yaunda kikosi kukabili majanga

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanajeshi wa Uganda

Jeshi la Uganda, limeweka vituo vya kukabiliana na majanga na dharura, ili kuharakisha shughuli ya kuwatuma wanajeshi wake haraka endapo kutatokea dharura au mzozo katika kanda ya Afrika Mashariki.

Wanajeshi wa Uganda, wamekuwa wakiwasaidia wanajeshi wa Sudan Kusini kupambana na wapiganaji wa waasi, kwa muda wa mwezi mmoja uliopita.

Mwandishi wa BBC mjini Kampala amesema kuwa huenda serikali ya nchi hiyo ikashirikishwa katika majukumu kama hayo siku zijazo.

Wanajeshi wa Uganda vile vil vile wanatunza amani nchini Somalia na Jamuhuri ya Afrika ya Kati.

Wanajeshi hao pia wamewahi kuhudumu katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda.

Muungano wa Afrika umekuwa na mpango wa kuunda kikosi maalum cha kukabiliana na majanga na mizozo, lakini pendekezo hilo halijaidhinishwa na vingozi wa serikali za nchini wanachama wa muungano huo wa AU.