Justin Bieber akamatwa na polisi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bieber alikamatwa Alhamisi asubuhi akiwa mlevi

Mwanamuziki mashuhuri duniani Justin Bieber,amekamatwa na polisi nchini Marekani kwa kosa la kuendesha gari akiwa mlevi.

Polisi katika mji wa Miami Beach, wamesema kuwa mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 19 pia alikuwa anaendesha gari lake kwa kasi kupindukia.

Mtandao unaofuatilia maisha ya wasanii wa kimataifa, TMZ umeripoti kuwa Justin Bieber aliondoka klabuni mapema asubuhi akiwa anaendesha gari aina ya Lamborghini wakati polisi walipomtaka kutumia kifaa cha kupima ikiwa alikuwa mlevi.

Alipatikana kuwa mlevi ndio maana akakamatwa.

Wiki jana polisi walifanya msako katika nyumba ya mwanamuziki huyo, baada ya madai kuwa alirusha Mayai katika nyumba ya jirani yake na kusababisha uharibu wa thamani ya maelfu ya dola.