Polisi 5 wauawa Misri

Haki miliki ya picha AP
Image caption Polisi wapambana na ghasia mjini Cairo

Maafisa watano wa polisi wameuawa nchini Misri baada ya kushambulizi na watu wenye silaha katika kizuizi kimoja cha polisi jijini Cairo.

Wengine wawili walijeruhiwa katika mji wa Beni Suef.

Washambulizi waliokuwa kwenye pikipiki walifyatua risasi na kisha kutoroka mahali hapo.

Msemaji wa polisi alidokeza kuwa wanawasaka washukiwa wa shambulio hilo.

Karibu maafisa wa usalama 250 wameuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na watu waliojihami tangu aliyekua Rais wa nchi hiyo Mohammed Morsi, kupinduliwa na jeshi Julai, mwaka uliopita.