Serikali ya SudanK yadai vita havikusita

Wapiganaji wa Sudan Kusini

Serikali ya Sudan Kusini imewashutumu waasi kuwa wamevunja makubaliano ya kusitisha mapigano, saa chache baada ya mkataba kuanza kutekelezwa.

Waziri wa habari, Michael Makuei Leuth, alisema maeneo ya serikali bado yanashambuliwa na alionya kuwa serikali huenda ikalazimika kujihami.

Pande hizo mbili katika vita vya Sudan Kusini zimekubaliana kusitisha mapigano kumaliza mapambano ya wiki tano ambayo yameuwa maelfu ya watu.

Makubaliano ya kusitisha mapigano yalitiwa saini Alkhamisis, lakini yalianza kutekelezwa saa 24 baadae.

Waziri Lueth hakueleza mapigano hayo yanatokea wapi nchini, lakini kulikuwa na mapambano Ijumaa katika jimbo la Jonglei.