Mahasimu wa Syria kukutana Geneva

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Serikali na upinzani Syria zinatarajiwa kukutana ana kwa ana kwa mara ya Kwanza Geneva

Waakilishi wa serikali ya Syria pamoja na makundi yanayompinga Rais wa taifa hilo Bashar Al Asaad, baadaye hii leo wanatarajiwa kukutana katika chumba kimoja kwa mara ya kwanza katika mazungumzo ya amani yanayoendelea mjini Geneva.

Wajumbe hao bado hawaja-jianda kufanya mazungumzo ya ana kwa ana,lakini mpatanishi wa umoja wa mataifa Lakhdar Brahimi amesema ana matumaini kwamba baada ya kuwaanda watazungumzia kuhusu maswala muhimu.

Inatarajiwa kuwa pande zote mbili zitakubaliana kuhusu maswala muhimu kama vile misaada kuwafikia raia walio katika mji uliozingirwa na vita wa Homs.