Tunisia yapata katiba mpya

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hii ni katiba ya kwanza kuidhinishwa tangu Ben Ali kuondolewa madarakani

Bunge la Tunisia limeidhinisha katiba mpya,ikiwa ni ya kwanza tangu kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo Ben Ali, yapata miaka mitatu iliopita.

Spika wa bunge hilo Mustapha Ben Jaafar ameitaja katiba hiyo kama mojawapo ya makubaliano yaliyoafikiwa kwa mustakabali mwema wa Tunisia.

Mwandishi wa BBC nchini humo anasema kuwa wanasiasa wana imani ya kutuma ujumbe wa udhabiti na umoja kwa raia wa taifa hilo pamoja na jamii ya kimataifa.

Wakati huohuo waziri mkuu nchini humo Mehdi Jomaa amesema ameunda serikali mpya.

Baraza la mawaziri linashirikisha wataalam na watu wasioegemea upande wowote wa kisiasa, linatarajiwa kuongoza serikali hadi uchaguzi mpya utakapofanyika.

Mehdi Jomaa alichaguliwa kama waziri mkuu mnamo mwezi Disemba,baada ya serikali ilikuwa ikiongozwa na chama cha Ennahda kukubali kujiuzulu kufuatia ongezeko la hali ya wasiwasi kati yake na upinzani wenye misimamo wa kadri.