Bilawal Bhutto ajipigia debe Pakistan

Haki miliki ya picha
Image caption Bwana Bilawal Bhuto Zardari anasema ataingia siasa mwaka 2018

Bilawal Bhutto Zardari, mwana wa kiume wa aliyekuwa waziri mkuu wa Pakistan Benazir Butto aliyeuwawa, ametoa wito kwa wanasiasa nchini wa Pakistan kuweka maanani juu ya tishio linatokana na uwepo wa makundi ya wanamgambo nchini humo, likiwemo kundi la Taliban.

Katika mazungumzo ya kipekee na BBC, bwana Bhutto amesema kuwa angependa kuliangamiza kabisa kundi la Taliban nchini Pakistan, na kutoa wito wa kampeni ya kijeshi dhidi ya kundi hilo.

Bwana Bhutto amesema kuwa wanasiasa wamepunja makubaliano yaliyojengwa na marehemu mama yake, kwa kuamini kwamba Marekani inapaswa kupigana dhidi ya kundi la Taliban kwa niaba yao.

Amesema anawazia kuingia siasa katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka 2018.