16 kizimbani kwa ugaidi Rwanda

Haki miliki ya picha
Image caption Mwanasiasa wa upinzani Victoire Ingabire amefungwa jela kwa kupinga serikali ya Kagame

Watu 16 nchini Rwanda wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kupanga njama ya ugaidi.

Washitakiwa ni pamoja na aliyekuwa mlinzi wa Rais Paul Kagame (Joel Mutabazi).

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamekuwa yakielezea wasiwasi kuhusu tisho dhidi ya maisha ya wapinzani wa serikali ya Kagame.

Awali afisaa mmoja mkuu katika Umoja wa mataifa, amekosoa ambavyo serikali ya Rwanda inawatendea wanasiasa wa upinzani.

Akiongea na BBC, wiki moja baada ya ziara yake nchini humo, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa, Maina Kiai alisema kuwa karibu kila mwanasiasa, anayejitokeza hadharani kupinga serikali, huishia kwenye matatizo ya kisheria.

Baadhi hukamatwa na kufungwa jela kwa kile kinachosemekana kuwa kueneza uvumi.

Bwana Kiai alisema kwamba alizungumza na mwanamume mmoja akiwa gerezani kuhusu siasa.

Kiai amesema kuwa angali anafanya mazungumzo ya kina na serikali ya Rwanda kuhusu hilo.