Wafungwa wa kisiasa wa S.Kusini huru

Wafungwa 7 wa kisiasa wameachiliwa huru na serikali ya Sudan Kusini.

Saba hawa ni kati ya wanasiasa wakuu 11 waliokamatwa wakati wa vurugu za kisiasa zilizotokana na njama ya mapinduzi iliyotibuka nchini humo Disemba mwaka jana.

Kenya imekubali kuwapa hifadhi wanasiasa hao. Wanaume hao saba waliandamana na Rais Uhuru Kenyatta kwenye mkutano na waandishi wa habari katika ikulu ya Rais mjini Nairobi.

Wanasiasa wengine wanne wangali wamezuiliwa nchini Sudan Kusini.

Mustakabali wa wafungwa hao ulikuwa kikwazo katika juhudi za amani kati ya waasi na serikali ya Rais Salva Kiir.

Pande hizo mbili zilitia mkataba wa kusitisga vita mwishoni mwa wiki jana na na kuahidi kusitisha vita ingawa duru zinasema kuwa hakuna upande umeaha kupigana.