Tahadhari: Pombe inaleta saratani

Haki miliki ya picha d

Wanasayansi wanaamini kuwa unywaji mwingi wa pombe unaweza kuleta hisia zisizo za kawaida mwilini ambazo zinaweza kuiweka ngozi katika hatari zaidi ya kupata Saratani ya ngozi.

Kemikali ya Ethanol inapogeuzwa kuwa “Acetaldehyde” baada ya ulaji wa chakula,kemikali hii yaweza kuiwezesha ngozi kupenyeza miale hata ya jua (UV light)

Watafiti waliofanya ugunduzi huo, nchini Uingereza wanakubali kwamba kuna mambo mengine yanayochangia mtu kupata Saratani ya Ngozi.

''Utafiti umeonyesha kuwa wagonjwa wanaougua Melanoma huathirika kwa ajili ya kuota jua kwa muda mrefu,hili linaweza kupunguzwa iwapo mtu atajikinga kutokana na jua kali,'' asema Sarah Williams wa Utafiti wa Kansa, Uingereza.

Kulingana na utafiti wao uliochunguza mada 16 tofauti na kushirikisha maelfu ya watu,unywaji wa chupa moja ya pombe moja au zaidi kila siku huongeza uwezekano wa kupata Saratani ya ngozi kwa asilimia ishirini.

Uwezekano wa kupata Saratani uliongezeka sawasawa na unywaji wa pombe,kwa mfano wale waliokunywa gramu 50 ya pombe walikuwa katika hatari zaidi ya kupata Saratani ya ngozi inayoua watu wengi zaidi duniani ,inayofahamika kama Melanoma.

Daktari Eva Negri,mmoja wa waandishi wa utafiti huu kutoka chuo kikuu cha Milan anasema kuwa unywaji wa pombe unaweza kuathiri uwezo wa mwili kujikinga hasa palipo na mnunurisho Wa miale ya jua.

Huu unaweza kuathiri seli kwa kiwango kikubwa na hivyo basi kusababisha Saratani ya ngozi.

Utafiti huu ulinuia kujua ni kwa kiwango gani pombe inachangia kuongeza uwezekano wa kuambukizwa Melanoma,na hivyo basi kuwepo kwa maarifa hii inaweza kuhamasisha watu kujikinga na miale ya jua.

Melanoma sanasana hujitokeza kwa mara ya kwa kwanza ngozini kupitia baka jeusi.

Profesa Chris Bunker,rais wa shirika la wataalamu wa ngozi nchini Uingereza alisema kwamba Saratani ya ngozi ndiyo kansa inayoripotiwa zaidi nchini Uingereza na inayowaua watu wengi zaidi nchini humo. Aliongeza kuwa utafiti wowote kwa swala hili unakaribishwa.

Wananchi wa Uingereza hufahamika sana kama wanywaji wa pombe na wenye kupenda kuota jua, hivyo basi utafiti huu utawaruhusu watu kufanya maamuzi bora kuhusu afya zao.

Melanoma

Dalili ya kwanza ya Melanoma ni kuwepo kwa baka jeusi ngozini au kubadilika kwa baka lililokuwa tayari kwenye mwili.

Hili laweza kufanyika katika sehemu yoyote mwilini hata hivyo miguu,mikono na uso huathirika pakubwa.

Kwa mara nyingi Melanoma huwa na umbo tofautitofauti na rangi zaidi ya moja.

Yaweza kuwa kubwa na mara kwa mara huwasha na kuvuja damu.

''Tunawahimiza watu kujitunza wanapokuwa chini ya miale ya jua .Kwa kuwa watu wengi hupenda kunywa mara kwa mara wanapobarizi, lengo letu ni kuwahamasisha kutahadhari na kukinga ngozi zao kila wakati.''

Mara nyingi baada ya kuota jua wakati wa likizo, wengi hubambuka ngozi.

Mtaalamu Sarah Williams wa shirika la utafiti wa SarataniKansa anasema kuwa uchunguzi huu hauelezi kikamilifu kinachosababisha Melanoma.

Hii ni kwa kuwa watafiti wenyewe wanaeleza kuwa, matokeo hayo ni kwa ajili ya miale ya jua wala si pombe. Utafiti nao umeonyesha kuwa Melanoma inatokana na kuota jua kwa muda na kubambuka ngozi:unaweza kujikinga kwa kujikinga na jua.

Kulingana na uchunguzi wake,jua nchini Uingereza halina nguvu zaidi kusababisha Sarataniy a ngozi, hata hivyo usisahau kukinga ngozi yako unapokwenda kupata jua wakati wa majira ya baridi.

Na kugusia swala la pombe na Saratani ya ngozi, ni muhimu kupunguza kiwango cha pombe unachokunywa. Pombe imetajwa kusababisha aina saba za kansa hivyo basi, Kupunguza unywaji yaweza kupunguza uwezekano wa kuambukizwa Saratani ya ngozi.