Jambazi sugu asakwa Tanzania

Image caption Ramani ya TZ

Polisi Nchini Tanzania wanamsaka mtu mmoja mwenye silaha, ambaye amewauwa watu wanane kwa kuwapiga risasi na kuwajeruhi wengine watatu.

Kisa hicho cha mauaji kilifanyika Jumamosi usiku katika eneo la Mara kaskazini.

Walioshuhudia wanasema kuwa jamaa huyo alikuwa akitaka kupewa pesa na simu za mkononi toka kwa waathiriwa.

Kikosi maalum kinachojumuisha maafisa wa polisi wapatao 160 kimekabidhiwa majukumu ya kumsaka jambazi huyo kwa nia ya kumtia mbaroni.

Mwanahabari wa BBC Nchini Tanzania anasema kuwa sio kawaida kwa watu wa Mara wanaopakana na Ziwa Victoria kubeba bunduki katika harakati za kulinda mifugo wao.