IGAD:Waangalizi kuenda S. Kusini

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanajeshi wa Sudan Kusini

Shirika la kikanda la IGAD la mataifa yaliyo katika upembe mwa Afrika, limeamua kuwa waangalizi wanapaswa kwenda nchini Sudan Kusini kuhakikisha kuwa mkataba wa kusitisha mapiganop unatekelezwa.

Uamuzi ulifikiwa katika mkutano wa Muungano wa Afrika unaondelea mjini Addisa Ababa Ethiopia.

Makabiliano makali yameendelea kuripotiwa nchini humo, licha ya mkataba wa amani kutiwa saini wiki jana kati ya waasi na serikali.

IGAD pia imetoa wito wa kuondolewa kwa wanajeshi wote wa kigeni nchini humo.

Hata hivyo, waziri wa mambo ya nje wa Uganda, Sam Kutesa, amesema kuwa Uganda haina mipango ya kuondoa wanajeshi wake ambao wamekuwa wakisaidia majeshi ya Sudan Kusini kupambana na waasi nchini humo.