TZ: Wabunge wajipa 'mkono wa kwaheri'

Image caption Kikao cha bunge la TZ

Kumekuwa na ghadhabu nchini Tanzania kufuatia uamuzi wa wabunge kujiongeza maelfu ya dola kama marupurupu.

Pesa hizo wanasema ni mkono wa kwaheri.

Marupurupu hayo yatatolewa kwa kila mbunge wa bunge la Tanzania lenye wabunge 357 wakati watakapokamilisha muhula wao wa tano kama wabunge.

Kila mbunge nchini Tanzania, hupokea mshahara wa dola elfu saba kila mwezi.

Wakazi wa mji mkuu Dar es Salaam waliambia BBC kuwa wameshtushwa sana na marupurupu hayo hasa baada ya kuambiwa na serikali kuwa hakuna pesa za kutosha kwa matumizi ya huduma za jamii.