EU yaonya kuhusu ufisadi Ulaya

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mwanaharakati Ulaya

Kamishna wa bara ulaya anayesimamia maswala ya ndani ya bara hilo ameonya kuhusu viwango vya juu vya ufisadi miongoni mwa nchi wanachama wa bara hilo.

Katika taarifa aliyoandika katika gazeti moja la nchini Sweden,Cecila Malmstrom amesema kuwa Ufisadi unaondoa uaminifu katika taasisi nyingi za kidemkrasia,kuharibu uchumi na kujenga mazingira yanayokuza uhalifu.

Amesema kuwa ufisadi umesababisha gharama ya hadi dola millioni 160 kwa mwaka.

Amesema kuwa tatizo hilo limekuwa likitokea katika mataifa tofauti na kwamba hakuna ambalo halijaathirika .