Huwezi kusikiliza tena

Mwanaharakati wa kwanza DRC

Mapema miaka ya elfu moja na mia tisa, mmishionari Alice Seeley-Harris kutoka Uingereza alifanya kampeni ya kwanza kabisa kwa kutumia picha, ili kupambana na ukiukwaji wa haki za binaadam.

Alionyesha ukatili wa utawala wa Mfalme Leopold wa pili wa Ubelgiji, ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Picha hizo sasa zipo katika maonyesho hapa London, zikionyeshwa kwa pamoja na mpiga picha kutoka Kongo Kinshasa Sammy Baloji.

Salim Kikeke alitembelea maonyesho hayo.