Miili 3 yapatikana Amazon Brazil

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Amazon

Polisi katika jimbo la Amazon nchini Brazil wamepata mabaki ya miili ya wafanyikazi wa serikali watatu ambao waliripotiwa kutoweka mwezi Desemba. Tayari jamaa ya waathiriwa wametambua miili yao.

Haki miliki ya picha Reuters

Eletrobras

Wenyeji watano kutoka kabila la Tenharim wameshtakiwa kwa kutekeleza mauaji hayo lakini wakakanusha mashtaka.

Mashirika ya kijamii katika eneo hilo yanadai wafanyikazi hao wa kampuni ya umeme ya Eletrobras waliuawa na wenyeji kulipiza mauaji ya kiongozi moja wa kabila hilo mwezi Desemba.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption wenyeji wa Amazon

Serikali ililazimika kutuma vikosi vya usalama kurejesha hali ya utulizu katika mji ulioko karibu wa Humaita baada ya maandamano makubwa kupinga mauaji hayo.