Hoffman alikuwa na mifuko '70' ya Heroin

Haki miliki ya picha AP
Image caption Phillip Hoffman

Polisi mjini New York, wamepata mifuko sabini ya dawa ya kulevya ya Heroin ndani ya nyumba ya muigizaji mahiri Hollywood, Philip Seymour Hoffman.

Vyombo vya habari nchini Marekani vinasema kuwa muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 46, alipatwa akiwa na mifuko 70 ya Heroin nyumbani kwake katika eneo la Greenwich.

Hoffman aliyefariki siku ya Jumapili, alipatwa akiwa na bomba la sindano kwenye mkono wake.

Uchunguzi wa madaktari ulifanywa Jumatatu ngawa matokeo bado. Polisi wanaamiini kuwa Hoffman alifariki kutokana na 'kujibwenga' kiwango kikubwa cha dawa hiyo.

Muigizaji huyo alipata kuteuliwa mara tatu kwa kazi yake nzuri ya uigizaji mjini New York.

Hoffman ameacha mke na watoto watatu. Katika ujumbe wao , familia ya Hoffman ilisema kuwa imesikitishwa sana na kuwa ni pigo kubwa kwa familia nzima kumpoteza.

Uchunguzi utabaini kilichomuua Hoffman punde baada ya kujidunga dawa ya Heroin.

Watu wanne wamekamatwa huku polisi wakiendelea na uchunguzi kuhusiana na kifo chake.

Mifuko mingine 350 ilinaswa na polisi wakati wa uchunguzi wao. Inaarifiwa Hoffman alikuwa anatumia dawa za kulevya tangu siku zake chuoni ingawa alikuwa ameacha kuzitumia kwa karibia miaka kumi.