Ufaransa kuteketeza pembe za Ndovu

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Biashara haramu ya pembe za Ndovu hufaidi zaidi Bara Asia

Tani tatu ya pembe za Ndovu zitateketezwa hii leo Nchini Ufansa ili kuonyesha kujitolea kwa serikali ya taifa hilo katika vita dhidi ya biashara hiyo haramu.

Wizara ya mazingira itatekeleza uchomaji huo wa shehena ya pembe za Ndovu zilizonaswa katika uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle.

Ufaransa ni taifa la kwanza barani Uropa kuharibu na kuchoma hadharani pembe haramu za Ndovu.

Muungano wa kimataifa wa uhifadhi wa mazingira, umesema kwamba takriba ndovu elfu 22 mwaka 2012.

Pembe haramu za ndovu huuzwa sana Nchini China na kwingineko barani Asia.

China ndio taifa kubwa lenye kufaidi kutokana na biashara haramu ya pembe za Ndovu