Wimbi la ghasia nchini Bosnia

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maelfu wanadai ajira na kupinga ufisadi

Maafisa nchini Bosnia wanasema kuwa takriban watu 200 walijeruhiwa siku ya ijumaa wakati wa ghasia nchini humo.

Majumba ya serikali katika miji kadhaa yalivamiwa na kuchomwa.

Katika mji mkuu wa Sarayevo ,maafisa wa polisi walitumia risasi za mipira pamoja na maji dhidi ya maelfu ya waandamanaji waliozichoma afisi za utawala wa eneo hilo huku wakijaribu kulivamia jengo la rais.

Maandamano hayo dhidi ya ukosefu wa ajira na ufisadi ni mabaya zaidi tangia mwisho wa vita vya Bosnia miongo miwili iliopita.

Maandamano yalianza katika mji wa Tuzla mapema juma hili kufuatia kufungwa kwa viwanda kabla ya kuenea.

Moshi mweusi ulionekana ukifuka kutoka katika jumba lenye ofisi za Rais mjini Sarajevo.

Kutokana na sifa yake ya kivita, watu wachache sana nchini Bosnia wana matumaini madogo sana ikiwa mageuzi yanaweza kufanyika nchini humo.

Kadhalika kutokana na hali hiyo, watu wamekuwa na ghadhabu sana na sasa wameanza kudhihirisha hasira yao.

Mnamo siku ya Alhamisi makabiliano kati ya polisi na waandamanaji yalisababisha majeruhi zaidi ya 130.