Mafuriko yaleta uharibifu Uingereza

Image caption Maelfu ya watu wamelazimika kuhama makwao kutokana na mafuriko

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron,amesema kuwa pesa sio hoja wakati huu ambapo watu wanahitaji msaada wa dharura huku baadhi ya sehemu za nchi hiyo zikikumbwa na mafuriko.

Baada ya kuzuru eneo la Kusini mwa England, ambako mafuriko yamesababisha uharibifu mkubwa, bwana Cameron amesema kuwa atafutilia mbali ziara yake ya Mashariki ya kati wiki ijayo ili ahakikishe kuwa hali inashughulikiwa vilivyo.

Alilaumu kile alichotaja,msimu mbaya wa baridi ambao umekuja na mvua kubwa kuwahi kushudiwa katika kipindi cha miaka 250.

Alionya kuwa hali huenda ikawa mbaya zaidi.

Mafuriko haya yamesababisha uharibifu wa zaidi nya nyumba elfu moja huku maelfu wakilazimika kuhama makwao.

Usafiri pia umetatizika.