Mhuburi aomba radhi baada ya kuzini

Image caption Kasisi Maina alisema tayari ameomba msahama kwa Mungu wake

Mhubiri mmoja mkristo nchini Kenya ameomba msamaha kanisani baada ya kupatikana akila uroda na mke wa mwanamume mwingine mjini Nyeri eneo la Kati mwa Kenya.

Mhubiri huyo alipangisha chumba katika mkahawa mmoja mjini humo, ingawa hakujua kuwa alikuwa amefuatwa na waandishi wa habari waliompata katika kitendo hicho na mke wa watu.

Alisema kuwa mbali na kutaka msahama wa waumini wa kanisa lake pia ameomba msamaha kwa Mungu.

Lakini huku wakazi wa Embu anakotoka kasisi huyo, wakitafakari msamaha kwa mhubiri huyo, viongozi wa kanisa anakotumikia wamemwachisha kazi kwa muda wakifanya uchunguzi kuhusu kashfa hiyo.

Kasisi Anthony Maina alijitokeza hadharani na familia yake baada ya maombi siku ya Jumapili na kutaka viongozi wa kanisa hilo la Assemblies of God kumsamehe kwa kuzini na mke wa wenyewe.

Mkewe mhubiri huyo na wanao walisema kuwa wamemsamehe kwa kile alichofanya.

Akiongea na waandishi wa habari, muhubiri huyo alisema kuwa hakwenda kanisani mjini Embu kujitetea.

Alikiri kuwa amemkosea Mungu na kusema kuwa tayari ameomba msamaha kutoka kwake.

Mmoja wa viongozi wa kanisa hilo alisema wakati kunatokea kitendo kama hiki, kasisi huondolewa katika majukumu yake kwa muda kabla ya kurejeshwa kazini.

Askofu mkuu wa kanisa hilo aliwasihi wananchi kutofurahia wakati, mtu anapopatikana na mkosi kama huo