Maelfu wahama kutokana na Volcano Indonesia

Haki miliki ya picha AP
Image caption Watu wakihama baada ya mlima Kelud kulipuka

Watu laki mia mbili wamehamishwa kutoka makwao kisiwani Java Nchini Indonesia, baada ya milipuko miwili ya volkeno kuutikisa mlima wa Kelud.

Majivu ya volkeno yamerushwa kutoka kilele cha mlima huo na kusambaa eneo kubwa Mashariki mwa Java na ripoti zinasema kuwa majivu ya volcano ya centimita tano yalianguka ardhini.

Viwanja vikuu vya ndege mjini Surabaya, Solo na Jogyakarta vimefungwa kwa sababu majivu hali yametanda angani na hivyo kusababisha hali ambayo marubani wa ndege hawataweza kuona mbali na pia tishio la kuharibu injini ya ndege.

Kufikia sasa utawala wa nchi hiyo umesema kuwa hakuna aliyekufa kutokana na mlipuko huo wa volkeno.

Mlipuko wa volkeno uliotokea katika mlima huo mwaka wa 1568,ulisababisha vifo vya maelfu ya watu.