Uhispania motoni kuhusu wahamiaji

Haki miliki ya picha AFP
Image caption wahamiaji haramu

Tume ya bara ulaya imesema kuwa itaitaka serikali ya Uhispania kuelezea ni kwa nini maafisa wa polisi walitumia risasi za mipira dhidi ya kundi la wahamiaji wa Afrika katika eneo lake la Cueta waliokuwa wakiogelea kutoka nchini Morrocco.

Takriban watu 14 walikufa maji wakati wa tukio hilo lililotokea juma moja lililopita.

Kamishna wa bara Ulaya anayesimamia maswala ya ndani Cecillia Malmstrom amesema kuwa hatua zozote zitakazochukuliwa na nchi za Ulaya kutetea mipaka yake lazima zieleweke.

Waziri wa maswala ya ndani nchini Uhispania amekiri kwamba risasi za mipira zilirushwa,lakini akasisitiza kuwa hakuna aliyepigwa na kwamba risasi hizo hazikusababisha vifo vya waliokufa maji.