Ndege ya Ethiopia ''Yatekwa Nyara''

Ndege ya abiria ya shirika la ndege la Ethiopia iliyokuwa ikisafiri kutoka Addis Ababa hadi Rome Italia ,imetekwa nyara na kulazimishwa kubadili mkondo wake na kutua mjini Geneva Uswisi. Katika taarifa kwa vyombo vya habari shirika hilo linasema kuwa abiria wote wako salama . Ndege hiyo imetua Geneva kulingana na msemaji wao katika uwanja huo wa ndege. Haijulikana hadi sasa ni nani aliyeiteka nyara ndege hiyo wala anataka nini. Tutakujuza habari zaidi pindi tutakapo aarifiwa .