Watu 10 wapoteza maisha Korea kusini

Haki miliki ya picha
Image caption Mfanyakazi wa kikosi cha uokoaji akiwa eneo la ajali,mjini Gyeongju

Takriban watu kumi wameuawa na zaidi ya 100 wamejeruhiwa baada ya jengo kuanguka nchini Korea Kusini.

Zaidi ya watu 560 wanaelezwa kuwa walihudhuria tamasha mjini Gyeongju walipoangukiwa na kufunikwa na sehemu ya Jengo.

Maafisa wanaeleza kuwa kati yao waliopoteza maisha, tisa walikua wanafunzi.

Kikosi cha uokoaji kimesema kuwa hali ya hewa na uzito wa barafu katika paa la jengo vimefanya shughuli za uokoaji kuzorota.

Wamekisia kuwa sehemu ya kati kati ya jengo ilishindwa kuhimili uzito wa barafu hali iliyosababisha kuanguka kwa jengo hilo.

Jengo lilianguka wakati wa tukio la utambulisho wa wanafunzi wa chuo kikuu wa mwaka wa kwanza kutoka mjini Busan.

Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa shughuli za uokoaji zinaendelea wakitafutwa walionasa kwenye vifusi.