Afueni kwa Wafanyikazi wa kigeni Saudia

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wafanyikazi wa kigeni Saudia

Saudi Arabia imeweka saini makubaliano na serikali ya Indonesia kwa lengo la kulinda haki za wafayikazi wa nyumbani kutoka Indonesia .

Wengi wa wafanyikazi wakigeni walioko Saudia hulalamikia kuteswa na kunyanyaswa kijinsia.

Wafanyikazi wengi hudai kuwa nyingi ya haki zao kukiukwa na waajiri wao mbali na kupokonywa vyeti vyao vya usafiri.

Kipengee muhimu cha makubaliano hayo ni kuwa wafanyikazi hao, wapatao millioni mbili hivi,hawatanyangang'wa hati zao za kusafiria wakiwa kazini na wala hawatazuiliwa kuwasiliana na jamaa zao.

Masharti mengine ni kuwa Watalipwa mishahara yao kwa wakati ufaao ,na kupewa mkataba wa kazi.