Bouteflika atagombea tena urais

Rais Bouteflika wa Algeria Haki miliki ya picha AFP

Waziri mkuu wa Algeria amesema kuwa rais mkongwe wa nchi hiyo, Abdelaziz Bouteflika, atagombea muhula wane kwenye uchaguzi wa mwezi Aprili ingawa kuna wasiwasi kuhusu afya yake.

Mwaka jana Bwana Bouteflika - mwenye umri wa miaka 76 - alipata ugonjwa wa kiarusi.

Alilazwa hospitali mjini Paris kwa miezi mine na hakuonekana hadharani tangu wakati huo.

Rais Bouteflika ameongoza nchi tangu mwaka wa 1999, wakati Algeria ilipokuwa ikipita katika vita vikali vya wenyewe kwa wenyewe baina ya serikali na wapiganaji Waislamu.

Waandishi wa habari wanasema Bouteflika ni kati ya viongozi wa mwisho waliobaki na ambao walipigana katika vita vya ukombozi kutoka kwa Ufaransa.

Ikifikiriwa kuwa mwezi Aprili atachukua fursa ya kukabidhi madaraka kwa kizazi kipya.